Friday, February 27, 2009

Vyakula Unavyopendelea

Sijui kuhusu ninyi, lakini mimi ninapenda chakula SANA. Ninahitaji chakula kula, bila shaka, lakini ninafurahia pia kuonja vyakula vya ajabu na kujaribu vyakula vipya. Ninapotafuta ladha ambayo sijawahi kula, ninajisikia kama kinywa kinakuwa hodari zaidi. Kwa mfano, leo usiku nilikula chokoleti na nyama ya nguruwe—nilishangaa, lakini ni tamu sana!

Hebu tuambie kuhusu vyakula unavyopendelea. Kuna chakula kimoja usingewahi
kutupa? Je ungeweza kula mlo umoja kwa maisha yote, ungekuwa kula nini? Tunda gani unapendelea? Na mboga gani? Nini chakula cha ajabu kuliko vyote ambavyo umekula? Ujibu maswali haya au utuambie hadithi nyingine kuhusu chakula. (Na tafadhali, uhakikishe huna njaa unapoandika au utahuzunika!)

Thursday, February 5, 2009

Kitabu cha burudani unachopendelea kukisoma.

Ukisoma Chuo Kikuu cha Stanford, unahitaji kupenda kusoma vitabu. Lakini, wanafunzi wa Stanford hawana saa ya kutosha kusoma vitabu kwa burudani. Je, kitabu gani cha burudani unapendelea zaidi? Ukipata wasaa, kitabu gani unataka kusoma badaaye?

Monday, February 2, 2009

Habari kutoka magazetini

Baada ya kusoma makala ya wiki hii kutoka IPP media umeona ni jinsi gani Rais Jakaya Kikwete amefanikiwa katika kusuluhisha migogoro iliyojitokeza katika nchi jirani mfano Kenya. Toa migogoro miwili amabayo ipo /imeshatokea katika jamiii yako na namna ya kuitatua.