Monday, May 25, 2009

Changamoto katika kujifunza Lugha.

Pengine, ni changamoto kuwasiliana katika lugha nyingine na watu wa utamaduni mwingine. Basi, utuambie kichekesho kuhusu kujifunza kufanya kitu au kusema kitu au kuelewa kitu katika Afrika Mashariki na katika Kiswahili. Chochote ni sawa, lakini ujaribu kutuchekesha! Kwa mfano, nafikiri niliwaambia watu wote kuhusu chakula cha asubuhi ambacho nilipika na sukari nyingi. Familia yangu ya Tanzania ilisema kilikuwa “kitamu sana!” lakini hawakukipenda na sikuelewa kwa sababu nilifikiri “tamu” ilifasiriwa “delicious” tu. Ninatumaini mimi si mtu pekee ambaye nimepata changamoto kama hii. Hebu tuelezee changamoto yako uliyokutana
nayo.

ku*wasiliana -to communicate

ku*fasiriwa -to be translated

Tuesday, May 19, 2009

Ungependa kukutana na nani katika maisha yako na kwa nini?

Ungeweza kukutana na mtu yeyote ambaye yuko hai au amekufa, ungechagua kukutana na nani na kwa nini?

Na Rachel

Tuesday, May 12, 2009

Kwa nini ungependa kuwa mtu maarufu?

Ukiwa na nafasi kujulikana, kwa nini ungependa kuwa maarufu? Kwa mfano, ujifanye kwamba ungeweza kufanya kitu chochote vizuri sana, na tafadhali usiseme ungekuwa kuwa mtaalamu mzuri, au ungefanya amani katika mahali pote, au kwamba ungewalisha watu wote. Bila shaka, vitu hivi ni muhimu, lakini ninapenda kufahamu tamaa nyingine zako kwa wewe mwenyewe tu. Je una heba za siri ambazo ungependa kuendeleza? Utuambie! Ukumbuke, hutakuwa fani tu, utakuwa mashuhuri sana. Nakutakia ujibu tofauti na majibu yaliyopita kuhusu pendekezo la utotoni na shughuli nyingine. Watu wengi watakufahamu, na namna ya washabiki wako itategemea juu ya sababu ya umashuhuri wako. Kwa hivyo, kwa nini kila mtu atajua jina lako?

Na Hilary

Msamiati:
ku*julikana -to be famous, in the limelight
maarufu -distinguished, famous
mtaalamu -scholar
heba -talents
fani -successful
mashuhuri -renouned, celebrated, illustrious
shughuli -career
umahuhuri -fame

Monday, May 4, 2009

Kumbukumbu ya Utotoni

Watu wote wana kumbukumbu nyingi kuhusu utoto wao, labda kuhusu likizo ya familia yao, au kuhusu shule ya msingi, au hata ndugu zao. Je, ni kumbukumbu gani uliyonayo kuhusu utoto wako unayoipenda zaidi? Ulikuwa mtoto mdogo wa umri gani? Ulikuwa mtoto mzuri, au mbaya? Ulifurahisha sana, au ulitasliti? Tueleze kuhusu utoto wako, tafadhali!

ku*tasliti - to stir up trouble

By Michelle.