Sunday, November 23, 2008

Sikukuu ya Thanks Giving

Habari za maandalizi ya sikukuu ya Thanks Giving.

Kwa kawaida sikukuu ya Thanks Giving ni muhimu sana kwa Wamarekani. Je, sikukuu hii chanzo (Source) chake ni nini?

Sunday, November 16, 2008

Mambo ya kufanywa na Rais Obama.

Hamjambo nyote?

Sasa uchaguzi wa marekani umemalizika na Barak Obama amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani. Rais Obama anatarajiwa na wananchi wa Marekani kufanya mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kurekebisha uchumi wa Marekani , huduma za afya pamoja na kulisafisha jina la Marekani.

Kwa mtazamo wako unaona ni mambo gani muhimu kumi ya kwanza ambayo Rais Obama angetakiwa aanze kuyafanya? Elezea mambo hayo kumi kwa kutumia kutendwa (Passive voice).

Thursday, October 30, 2008

Tofauti kati ya huduma za afya za afrika ya mashariki na hapa Marekani.

Katika muda ulioishi katika Afrika ya Mashariki, umeona tofauti gani zilizopo kati ya huduma za afya za Afrika ya Mashariki na za hapa Marekani? Toa maoni yako tafadhali.

Saturday, October 25, 2008

Tofauti kati ya maisha ya Afrika ya mashariki na Marekani.

Habari zenu,

Katika likizo yenu ya Kiangazi mlikwenda Afrika ya Mashariki na mliishi pale kwa miezi kadhaa. Je kuna tofauti gani kati ya maisha na utamaduni wa Afrika ya Mashariki na Marekani?

Toa maoni yako pamoja na misamiati utakayokuwa nayo katika mada hii.

Tuesday, October 14, 2008

HEKAHEKA ZA UCHAGUZI WA RAIS NCHINI MAREKANI

Hamjambo jamani?

Waswahili walisema, "Kila jambo lina mwisho wake". Ni siku chache tu zimebaki kwa wamarekani kumchagua Obama wa chama cha Democratic au McCain wa chama cha Republican kuwa rais wao.
Wewe kwa mtazamo wako, unadhani ni nani atashinda kuwa rais kati ya wagombeaji hawa wa wawili? Na kwa nini?