Saturday, January 31, 2009
Mipango ya Kiangazi kijacho
Kwa kawaida, wakati wa mwezi wa pili, wanafunzi huanza kufikiri kuhusu kiangazi kijacho. Kwani hatuna madarasa wala pesa, na tunahitaji kuendelea na utafiti wetu, na kupanga mapema. Je, ungependa kufanya nini ? Kwa nini unataka kusoma Kiswahili wakati wa kiangazi au sasa? Na je ni kwa vipi utatumia lugha hii? Tafadhali, eleza kuhusu mipango yako.
Saturday, January 24, 2009
Maisha Tofauti
Wakati mwingine nikiwaza kuhusu maisha yangu yanavyoendelea ninaona kwamba ni bora kama nisingalisoma historia ya Afrika Mashariki katika Chuo Kikuu cha Stanford na kwamba ningalikuwa msanii. Je mngalibadilisha maisha yenu mngalifanya nini? Je, mngalisoma Chuo Kikuu cha Stanford? Mngaliishii hapa nchini Marekani au katika nchi nyingine? Mngalifanya kazi nyingine? Tafadhali wazeni kuhusu maisha yenu. Je mngalichagua njia / mpango mwingine wa maisha tofauti na wa sasa?
Sunday, January 11, 2009
Tofauti kati ya biashara za zamani na za sasa baina ya Afrika ya Mashariki na sehemu za dunia nyingine
Kumekuwa na biashara kati ya watu wa Afrika ya Mashariki na sehemu za dunia nyingine (kama Arabian Peninsula au Southeast Asia) kwa miaka mingi. Je kuna tofauti gani kati ya ufanyaji wa biashara wa wakati huu na ule wa wakati uliopita (miaka mia moja iliyopita, kwa mfano).
Subscribe to:
Posts (Atom)