Friday, April 24, 2009

Unazitumiaje pesa zako?

Ninapopata pesa kidogo, kwa kawaida huzitumia kuwa na tajariba nzuri. Kwa mfano, hula pale hotelini tamu au husafiri katika nchi tofauti. Watu wananiambia kwamba nilinde pesa zangu kwa ajili ya wakati ujao ama ninunue nguo au vitu vingine. Je, unapopata pesa, huzilinda au huzitumia? Ukitumia pesa, unapendelea kununua vitu au kuzitumia kwa ajili ya tajariba maalum?

Na Lisa.

Tuesday, April 14, 2009

Sikukuu unayoipenda.

Kesho ni siku ya mwisho wa sikukuu ya Passover. Unapendalea sikukuu gani? Una dini? Ungeweza kutengeneza sikukuu, ungefanya nini?

Sunday, April 5, 2009

Mipango ya maisha

Ulipokuwa mdogo, ulikuwa ukifikiri kwamba ungefanya nini utakapokuwa mtu mzima? Kwa nini ulipenda kazi hii? Mara kwa mara, nilifurahia kukumbuka mipango yangu kutoka utoto, kwa sababa yananichekesha. Kwa mfano, pengine, nilitaka kuwa daktari ya macho. Nilihitaji degaga nilipokuwa mdogo sana, na kapenda lenzi ambaye wao hutumia kuangalia macho. Pengine, nilitaka kuendesha ndege. Nilijua majina ya kila ndege (nimeyasahau sasa) na kaangalia katika mbingu kuziona kila siku. Pengine nilitaka kuwa mwandishi pia. Nilikuwa nikiandika hadithi fupi kuhusu familia kubwa inayekaa katika jimbo la Texas (ingawa sijawahienda Texas)! Labda ndoto hii ni karibu na nususi, kwa sababu ninapaswa kuandika kitabu ili kupata shahada ya tatu. Nimefurahi kwamba sikusomo udaktari wa macho au jinsi kuendesha ndege. Vitu hivi vingenichokesha sana leo! Je, mipango yako yamebadilika tangu utoto? Ulipenda kufikiri kuhusu wakati ujao au hapana?

Msamiati:
degaga (9/10) eyeglasses
lenzi (9/10) lenses
mbingu (9/10) sky, heavens
nususi (9/10) fact, reality