Thursday, February 5, 2009

Kitabu cha burudani unachopendelea kukisoma.

Ukisoma Chuo Kikuu cha Stanford, unahitaji kupenda kusoma vitabu. Lakini, wanafunzi wa Stanford hawana saa ya kutosha kusoma vitabu kwa burudani. Je, kitabu gani cha burudani unapendelea zaidi? Ukipata wasaa, kitabu gani unataka kusoma badaaye?

4 comments:

Hilary said...

Nani alisemi siwezi kusoma vitabu kwa burudani? Nina sera ya thabiti kwamba nisome riwaya kila usiku kabla ya kulala. Mara kwa mara, wanafunzi wengi husoma kufanya kazi kitandani, lakini kanuni yangu ni kusoma vitabu kwa anasa kitandani tu. Ni muhimu kuhakikisha kwamba kila kitu si kazi, vinginevyo ubongo wako utakuondoka.

Kwahiyo, kujibu swali, napenda kusoma riwaya sana. Pambano tu ni kwamba kila wakati, mimi hutaka kuhukumu kitabu mujibu kifuniko. Napendelea kifuniko kizuri. Juu ya hivyo, najua ni bora nichague mujibu ubora wa kuandika na hadithi.

Pia, ukitaka kusoma kitabu kutoka nchi zingine, lazima uhesabu tafsiri. Kwa mfano, nilisikia kwamba Dostoevsky aliwachekesha watu wa Urusi, lakini nilipokisoma “Dhambi na Adhabu,” sikucheka. Halalfu, nilipata nakala ya “Kaka Karamazov” waliyoitafsiri watu wengine, na nilicheka sana! Najua mimi ni wa jibini, lakini, kwa sababu mimi ni mwanafunzi wa lugha, nafikiri tafsiri ni muhimu sana katika riwaya geni. Vitabu vengine ninavyovipenda ni hadithi fupi, kama hizo na Raymond Carver na waandishi kutoka kusini ya Marekani, kama Flannery O’Conner. Aidha, nafurahishwa na vitabu vya aina ya “hakika ya azima” kama hivyo na Gabriel Garcia Marquez na Zakes Mda. Labda siku moja, nitapokuwa mzee, nitaandika kidogo pia.


thabiti -undoubted, rigid, firm
riwaya (n-n-) -novel
kanuni (n-n-) -rule, principle
anasa (n-n-) -pleasure, enjoyment
mujibu -according to (adv)
kifuniko (ki-vi-) -cover, lid
ubora (w-) -excellence, quality
ku*hesabu -to consider
Urusi (w-) -Russia
dhambi (n-n-) -sin, crime
adhabu (n-n-) -punishment
nakala (n-n-) -copy
geni -foreign (adj)
hakika (n-n-) -reality
azima (n-n-) -magic

Michelle said...

Kwa kawaida, ninasoma kitabu cha historia ya Afrika, na muhula huu, nimesoma pia kuhusu historia ya ramani. Nikipata wakati kusoma kwa burudani, ninapenda sana kusoma riwaya ya kisayansi na vitabu vya uwezo wa kubuni. Kwa maoni yangu, kusoma vitabi kama vitabu hivi ni kama likizo! Vitabu hivi inasomeka, hivi ni rahisi sana kusoma. Kweli, mimi husoma kabla ya kulala kila siku, kwa sababu inanisaidia kulala haraka. Kwa kawaida, nimelala baada ya kusoma kurasa sita au saba tu!

Ninapendelea zaidi vitabu vya Orson Scott Card. Labda kitabu kinaonekana dufu, lakini kitabu ninapendelea zaidi kinaitwa Ender’s Game. Ni kuhusu mtoto ana hodari sana, na yeye anasoma kuwa kiongozi wa vita katika angani. Kitabu kinafuata mtoto, analewa na viongozi vingine katika chombo cha angani. Nimesoma ktabu hiki mara mingi, na nikipenda ijapokuwa ninajua tukio lijalo.

map - ramani
science fiction - riwaya ya kisayansi
fantasy - uwezo wa kubuni
seem - kuonekana
silly - dufu
outer space - angani
space ship - chombo cha angani
even though - ijapokuwa

Unknown said...

Ninafikiri kwamba wanafunzi wa Stanford hawana saa ya kutosha kusoma kwa jumla, sio vitabu kwa burudani tu. Ninapenda kusoma vitabu kwa burudani na kabla la kugundua anthropolojia, nilitaka kuwa mwandishi. Shuleni nilisoma na kuandika wakati wote na nilichagua chuo kikuu baada ya kufanya utafiti ili nitafuta chuo na mradi wa fasihi mzuri. Lakini nilipofika Columbia, nilifanya darasa la anthropolojia na niligundua kwamba nilitaka kuwa mwalimu wa anthropolojia katika chuo kikuu.

Sasa ni ngumu kutafuta saa kusoma vitabu kwa burudani kwa sababu nina orodha kubwa ya vitabu ninavyohitaji kusoma kwa tasnifu yangu. Ninapokuwa na wakati nje ya chuo (kama vile kiangazi) husoma vitabu vitoka orodha hiyo. Labda ninapaswa kubadilisha ama nitakuwa nikichoka hivi karibuni.

Wakati niliposoma kwa burudani zaidi, nilisoma aina za vitabu mbalimbali. Ninawapenda waandishi kama vile Jeanette Winterson, Virginia Woolf, Gabriel Garcia-Marquez na Marcel Proust. Ninaupenda mtindo wa kuandika unaoitwa “magical realism” kwa sababu ninapenda kujifanya kwamba vitu ajabu vinaweza kutokea. Pia ninapenda kusoma kuhusu mahali (miji, kwa mfano), halafu ninawapenda waandishi wanaoandika kuhusu mahali zaidi kuliko watu. Waandishi hawa ni Orhan Pamuk, Paul Auster na Rick Moody, kwa mfano.

Kuzungumza kuhusu kusoma kwa burudani kunisababisha kutaka kusoma zaidi!


Msamiati
tasnifu - dissertation
burudani – pleasure

Unknown said...

Ni kweli kwamba hatuna wakati wengi kusoma vitabu vya burundani kwa sababu sisi hatuna saa ya kutosha na sisi husoma vitabu vyingi kwa madarasa yetu. Kwa hivyo, nikipata wasaa ningesoma vitabu vya Henry Miller, Gunter Grass, na Hannah Arendt. Ningepata pia madarasa ya fasihi.

Vitabu vya hadithi ninavyopenda zaidi viliandikwa kwa watoto. Ingawa mimi si mtoto ninavipenda kwa sababu vinanikambusha ndoto. Vitabu vinaitwa “Bikari ya Dhahabu” (The Golden Compass), “Kisu ya “Subtle” (The Subtle Knife; Nina tatizo la kutafsiri), na “The Amber Spyglass” (Sijui kuitafsiri kabisa!). Mwandishi Philip Pullman aliviandika pamoja. Halafu kisa cha kila kitabu kinafuata kitabu cha mwisho kabla. Vitabu ni kuhusu mvulana na msichana wanaoishii ulimwengu tafauti. Wana wanyama wanaowafuata na wanajaribu kusaidia ulimwengu. Ni ngumu kueleza visa (hata kwa Kiingereza), lakini ninavipenda na ningefurahia kuvisoma tena. Vitu vya uchawi vyingi vinatokea.

Ninapendelea pia kitabu kinachoitwa “Ngoma ya Bati” (The Tin Drum) kinachoandikwa kwa Gunter Grass. Kisa kinatokea nchini Ujerumani wakati vita vya pili vya dunia. Ninakipenda pia “Dhambi na Adhabu” (Crime and Punishment).

Misamiati:
Fasihi: literature
Ndoto: dream
Bikari: compass
Mwandishi: author
Kisa: story
Hadithi: fiction
Kutokea: to occur
Dhambi: crime
Adhabu: punishment