Thursday, October 30, 2008

Tofauti kati ya huduma za afya za afrika ya mashariki na hapa Marekani.

Katika muda ulioishi katika Afrika ya Mashariki, umeona tofauti gani zilizopo kati ya huduma za afya za Afrika ya Mashariki na za hapa Marekani? Toa maoni yako tafadhali.

4 comments:

Unknown said...

Ingawa nilitembelea hospitali pale Afrika ya Mashariki, sijui vitu vingi kuhusu huduma za afya pale. Lakini, ninaweza kueleza kuhusu mazoea yangu katika mahali pa afya.

Nikiwa mgonjwa sana pale Nairobi, nilienda hospitali inayoitwa Aga Khan. Nilihitaji kuenda hospitali badala ya daktari, kwa sababu daktari ni ghali sana. Sijui kama watu pale Nairobi wana bima ya afya (health insurance?) au kama wanaweza kutumia bima ya afya ili watembelee daktari za kibinafsi kwa bei ya rahisi. Lakini, ningefikiri kwamba watu hawana bima ya afya kwa sababu marafiki zangu za Afrika ya Mashariki huenda duka la madawa wakiwa wagonjwa. Hawaendi hospitali au daktari.

Tuendelee habari za kutembelea hospitali. Nilipofika Aga Khan, nilihitaji kulipa kabla ya kutembelea muuguzi au daktari. Halafu, nilihitaji kusubiri kwa muda mrefu. Baadaye, niliitwa na muuguzi. Alipima shinikizo yangu ya damu, alipima joto, na aliniuulizia matatizo yangu. Baada ya vitu hivi, alinipelekea chumba cha kusubiri.

Hapa Marekani, wakati wote unalipa baada ya kutembelea daktari. Pia, kwa kawaida, baada ya kuzungumza na muuguzi, unasubiri katika chumba sawa hadi daktari hufika.

Turudi Aga Khan...Baada ya dakika nyingine, mtu mwingine aliniita. Nilihitaji kuenda chumba tofauti ambamo mtu (labda alikuwa muuguzi pia?) alinichukulia damu. Halafu, niliondoka chumba hiki na kusubiri pale chumba cha kusubiri tena.

Hapa Marekani, huhitaji kuhamisha kutoka mahali pa moja mpaka mahali pengine. Kwa kawaida, baada ya kuondoka chumba cha kusubiri, hurudi hadi umemalizia pale hospitali au ofisi ya daktari.

Turudi Aga Khan tena. Baada ya kusubiri tena, nilikutana daktari ambaye aliniambia nipumzike tu. Sikuwa na furaha kwa sababu hakunisaidia daktari na nilihitaji kusubiri tena! Hatimaye, baada ya saa moja, mtu aliyenichukulia damu kuniambia sikuwa mgonjwa kwa sababu sikuwa na "malaria". Kabla ya kuondoka hospitali, nilihitaji kutembelea na muuguzi tena (!!!) aliyeniuliza nikisikia bora. Halafu, baada ya masaa matano, niliondoka hospitali.

Hapa Marekani, kama niliandika juu, kwa kawaida huhitaji kusubiri kwa muda mrefu. Pia, unabaki katika chumba kimoja; muuguzi na daktari wanakujia chumba chako. Huhamisha sana kama pale Afrika ya Mashariki. Lakini, kama huna bima ya afya hapa, kutembelea daktari au hospitali ni ghali sana kuliko Afrika ya Mashariki. Halafu, kuna vitu vizuri vingi kuhusu huduma za afya hapa na pale pia.


Msamiati Mpya
mazoea - experiences
shinikizo ya damu - blood pressure
kupima joto - to take someone's temperature
kuhamisha - to shift from, to move, to transfer
bima ya afya - health insurance?

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Katika muda nilioishii jijini Nairobi, niliona tofauti kati ya huduma za afya pale na za hapa Marekani. Lisa anayeishii pamoja nami tulipata homa. Tuliumwa matumbo na vichwa. Tuliogopa kuwa malaria halafu tulinia tuende katika Hospitali Aga Khan kupimwa. Lakini hatukujua tungengoja masaa matano hadi mwisho wa ziara yetu.

Mosi tulimlipia mpokezi. Katika Marekani hulipa wakati wa mwisho wa ziara. Lakini siku yetu haikatokea kama nilivyofikiri. Tulihitaji kusuburi saa moja kumwona daktari.

Daktari alituambia tusiogopi. Alijaribu kututambulia lakini hakujua sababu tulikuwa wagonjwa. Tulipewa agizo la dawa lingeloacha maumivu wetu lakini hatukutaka kungoja kupata dawa.

Halafu ilitubidi kungoja tena kupigwa sindano ili ipimwe damu yetu kwa malaria. Tulijifunza hatukupata malaria. Daktari alituuliza tukipona. Tulimjaribu “ndiyo” kwa sababu baada ya kusubiri masaa matano tulipata nguvu na tulipata nafuu tu. Daktari hakutusaidia kupona.

Matibabu ya Hospitali Aga Kha si nzuri. Katika marekani haibidi kwenda mahali mengi katika hospitali kuonwa na daktari, kupewa dawa, na kupigwa sindano.


Msamiati:
Kunai: to intend, resolve
Kupima: to test, examine
Ziara: visit
Mpokezi: receptionist
Dawa: medecine
Maumivu: pain
Utambuzi: diagnosis
Kutambua: to diagnose
Kupiga sindano: to give an injection
Kupona: to heal, recover
Kupata nguvu: to gain strength
Kupara nafuu: to feel better
Utibabu/Matibabu: medical care

Michelle said...

Kweli kabisa - huduma za afya katika Afrika ya Masharika ni tofauti sana kuliko njia marekani, au hasa njia kanada. Kwanza, hakuna hospitali binafsi katika Kanada. Katika Marekani, kuna hospitali binafsi tu. Katika Tanzania, inategemea - Tanzania ina hospitali binafsi na hospitali serikali (nafikiri). Serikali Kanada inalipa kwa huduma za afya, basi ni bure kwa wananchi, na hasa serikali hainalipa bei ghali sana kama katika Marikani. Katika Marikani, ni tatizo kubwa ukikuwa bila jukumu, kwa ajili ya bei ya huduma za afya ni juu sana.

Nilitembelea hospitali binafsi tu nilipokuwa katika Tanzania - rafiki yangu ilikuwa mgongwa, halafu tulienda Aga Kahn, imo mjini. Katika hospitali hii, huduma ilikuwa harakaharaka kuliko huduma za Kanada. Doktari hapo aliona rafiki yangu baada ya muda fupi sana, kama dakika tano tu. Nilikuwa na wasiwasi, kwa sababu nilikuwa na dolla mia moja mfukoni.

Lakini, tulikuwa na bahati nzuri. Bei kwa jumla ilikuwa dolla mia moja, kamili! Rafiki yangu haikuwa jukumu, lakini tulikuwa na pesa kutosha kulipa. Huduma wa hospitali ilikuwa nzuri sana. Najua Aga Kahn ni ghali sana kwa watanzania, na bei hapo ni mno kwa watanzania kwa jumla. Halafu, napenda mfumo mkanada nzuri zaidi. Watu wote wanalipa ushuru, na watu wote wanaweza kwenda hospitali bure. Nafikiri mfumo huu ni adili zaidi.

jukumu (5-6) - insurance (also guarantee, warranty)
wasiwasi (14) - worry
mfumo/mifumo - system(s)
adili (agj) - impartial, just, righteous