Saturday, January 31, 2009

Mipango ya Kiangazi kijacho

Kwa kawaida, wakati wa mwezi wa pili, wanafunzi huanza kufikiri kuhusu kiangazi kijacho. Kwani hatuna madarasa wala pesa, na tunahitaji kuendelea na utafiti wetu, na kupanga mapema. Je, ungependa kufanya nini ? Kwa nini unataka kusoma Kiswahili wakati wa kiangazi au sasa? Na je ni kwa vipi utatumia lugha hii? Tafadhali, eleza kuhusu mipango yako.

4 comments:

Unknown said...

Mimi nina wasiwasi kuhusu kiangazi kijacho, kwa hivyo ninajaribu kutofikiria. Lakini, kwa sababu umeniuliza, ninajaribu kueleza....

Ningependa kufanya mradi wa GPA pale Arusha, Tanzania. Mradi unaanza mwisho wa mwezi wa Juni na unamaliza mwisho wa mwezi wa Agosti. Katika mradi, ningesoma Kiswahili kwa masaa manne kila siku na kutembelea mahali muhimu kama vile Ngorongoro Crater, Zanzibar, na kadhalika. Ninataka kusoma Kiswahili kwa sababu ninafanya utafiti kuhusu uhusiano baina ya nchi ya Kenya na mji wa Dubai.

Ninafurahishwa na Wakenya wanaosafiri kwenye Dubai ili wanunue vitu safi au wafanye kazi pale. Pia ninataka kufahamu zaidi kuhusu jinsi Wakenya wanavyohisisha mji wa Dubai katika maisha yao. Ndiyo ni sababu baada ya kusoma Kiswahili pale Arusha, Tanzania ningependa kuenda Dubai ili nigudue watu na mahali nitakapotaka kufahamu wakati nitafanya utafiti pale. Sijawahi kuenda Dubai, kwa hivyo ninahitaji kutembelea pale nikitaka kufanya utafiti pale kwa mwaka mmoja au mwaka mbili kuanzia mwaka elfu mbili na kumi.

Lakini kama ningeenda Arusha na Dubai, nisingekuwa na wakati na mchumba wangu kwa sababu yeye anahitaji kukaa Marekani ili amalize utafiti wako kuhusu mji wa Memphis, Tennessee. Kiangazi kilichopita nilimkumbuka sana na ilikuwa ngumu kunuika mambo pale Kenya kwa sababu sikuweza kuzungumza naye juu ya mambo hayo. Kwa hivyo, kiangazi kijacho ikiwa sitasoma Kiswahili pale Arusha, Tanzania labda nitahudhuria mradi wa Kiswahili pale Michigan. Halafu, mchumba wangu anaweza kunitembelea nitakaposoma. Kuna tatizo ya pesa pia, lakini ni mambo kwa blogu nyingine...


kuhisisha – to incorporate, to associate, to involve
kunuika – to concentrate one’s thoughts on something

Rachel Quint said...

Nilipofika Marekani mwezi wa kwanza, nimepata wasiwasi sana pia kuhusu kiangazi kijacho. Kwa sababu nilikaa Tanzania, nimekwepa kufikiria kuhusu mipango yangu.

Lakini, nimeanza kutanganeza mipango. Mama na Baba yangu hawataka kwa mimi kurudi Afrika kwa sababu wanasema nimesharudi sasa hivyo na ninahitaji kukaa hapa Marekani kwa muda mfupi zaidi. Pia dada yangu mkubwa amesema anafikiri ninahitaji kupata kazi kweli. Halafu, nitajaribu kupata kazi hapa hapa Stanford.

Nimeandika uombi kwa kazi kwa Stanford. Ninataka kufanya kazi na kundi inaitwa Flora Family Foundation (FFF). FFF inafanya kazi kupata pesa kwa watu ambayo wanhitaji pesa katika Afrika Mashariki.

Ninafikiri kuna mkazo sana kuhusu mipango ya kiangazi kwa sababu wanafuzi wanafikiri hii ni nafasi basi kupata ujuzi!

Ninaamani ninaweza kupata kazi, na kupata mapumzikio pia!

Msamiati:
nafasi - time, opportunity
ujuzi - experience, expertise
kundi - group

Michelle said...

Kiangazi kijacho, nina mipango mengi. Ningependa kuenda Tanzania, kusoma Kiswahili tena. Pia, nitatafita kwa ajili was tasnifu yangu, kuhusu historia reli ya Tazara, kati kati ya Tanzania na Zambia. Nina mipango mingi kufanya vitu hivyo. Kwanza, ninajaza uombi mingi. Ningependa kwenda mji wa Arusha, kusoma Kiswahili na kozi “GPA,” itasoma katika taasisi TC-MCDC. Rafiki yangu, anaitwa Corinne, alisoma katika taasisi hii mwaka uliopita, na yeye alinieleza kwamba ilikuwa kozi nzuri zaidi, hata nzuri zaidi kuliko TUKI, labda. Nikishida, nitafanya Kiswahili na kozi GPA. Nikishindwa, natumaini kwamaba nitashinda pesa ya FLAS, na nitaweza kwenda Arusha kutumia pesa nyingine.

Baada ya kusoma Kiswahili kwa wiki nane, nitaenda nyaraka wa Tanzania (na labda nyaraka wa Zambia pia) kwa ajili ya kufanya utafiti. Utafiti yangu kulenda shabaha juu ya uzoefu wa akili na wa utendaji katika Tanzania muda baada ya uhuru, wakati wa kujengo ujamaa. Ni ghali sana kusafiri Afrika ya Mashariki, basi nikienda, nitafanya vitu vingi kazkasini kijacho.

uombi - application
taasisi (i-zi)- institution
nyaraka - archives
kulenda shabaha - to focus (on an objective)
uzoefu - experience
utendaji - practice

Unknown said...

Ni muhimu tufikiri kuhusu mipango yetu. Sasa ninafanya uombi ili niende nchini Tanzania kusoma Kiswahili au niende kwenye Chuo Kikuu cha Michigan kusoma Kisomali wakati kiangazi kijacho. Ninahitaji kusoma Kiswahili na Kisomali kwa sababu nitafanya utafiti kuhusu historia ya Wasomali wa Kenya. Nitawahoji kwa Kiswahili na Kisomali. Halafu ninahitajia kusoma lugha hizi ili kufanya mahojiano. Pia kuna hati na makala katika makavasi ya kitaifa ya Kenya zilizoandikwa kwa Kiswahili.

Nikienda Tanzania kiangazi kijacho nitasafiri nchini Uiingereza na Kenya. Ningefanya utafiti katika makavasi ya kitaifa ya Uiingereza jijini London na katika makavasi ya Kenya jijini Nairobi. Ninataka pia kuwagundua wasomali wazee ambao walikumbuka wakati ukoloni. Ninataka pia kuhakiki mahali ambapo nitafanya mahojiano.

Nitasoma pia vitabu vyingi ili nipange na niandae mitihani yangu. Mwaka ujao nitapimwa kuhusu ujuzi na elimu yangu ya vitabu vya umuhimu vya historia. Profesa wangu watataraji kwamba nitajua makala na vitabu vyingi vilivyoandikwa kwa Kifaransa na Kiingereza.

Msamiati:
Uombi: applications
Kuhoji: to interrogate, question
Mahojiano: interview
Hati: documents
Makavasi: archives
Kuhakiki: to determine
Kupimwa: to be tested
Ujuzi: experience, knowledge, expertise
Kutaraji: expect, hope