Friday, February 27, 2009

Vyakula Unavyopendelea

Sijui kuhusu ninyi, lakini mimi ninapenda chakula SANA. Ninahitaji chakula kula, bila shaka, lakini ninafurahia pia kuonja vyakula vya ajabu na kujaribu vyakula vipya. Ninapotafuta ladha ambayo sijawahi kula, ninajisikia kama kinywa kinakuwa hodari zaidi. Kwa mfano, leo usiku nilikula chokoleti na nyama ya nguruwe—nilishangaa, lakini ni tamu sana!

Hebu tuambie kuhusu vyakula unavyopendelea. Kuna chakula kimoja usingewahi
kutupa? Je ungeweza kula mlo umoja kwa maisha yote, ungekuwa kula nini? Tunda gani unapendelea? Na mboga gani? Nini chakula cha ajabu kuliko vyote ambavyo umekula? Ujibu maswali haya au utuambie hadithi nyingine kuhusu chakula. (Na tafadhali, uhakikishe huna njaa unapoandika au utahuzunika!)

4 comments:

Michelle said...

Ninakukubali, kabisa. Ninapenda chakula chochote. Kabla ya kuanaza digirii hii, nilikuwa nikikula mboga. Sikuwa mtu wa kula mboga, lakini kwa kawaida nilipendelea mboga, hasa nyanya, na mbilinganyi. Nilipokaa mji wa Halifax, nilikuwa nikitembelea soko la wakulima. Nilipofika jimbo la Kalifornia, nilichagua kujiunga “Two Small Farms” (“Mashambaa madogo mawili”). Kila wiki, Mashamaa Madogo Mawili nipa kasha kubwa, ulijaliwa na miboga mingi. Miboga ilikuwa tamu sana kuliko miboga ya Safeway!

Mwaka uliopita, niliamua kujifunza jinsi la kupika nyama pia. Nilipenda nyama, lakini kweli sikujua jinsi la kupika nyama kama kondoo au n’gombe. Kweli, nilijua jinsi la kupika kuku tu. Kwa Krismasi, nilianza na bata mzinga. Shangazi wangu anapika bata mzinga nzuri zaidi kuliko mama yangu, halafu shangazi wangu alinifundisha. Tulishinda - bata lilikuwa tamu sana. Niliporudi hapa, nilijaribu nyama nyingine.

Sasa, kusaidiwa na mchumba wangu, ninaweza kupika nyama ningi. Jana usiku, tulipika kondoo. Nyama niliyopendela ni kondoo.

Misimiati
-a kula mboga - vegetarian (adj)
mbilinganyi - eggplant
kasha - box
bata mzinga - turkey

Unknown said...

sNinapenda kula vyakula vya mpya na ajabu. Ninapenda kusafiri kwa sababu ninapenda kujaribu vyakula vya nchi zingine. Ninapenda chakula cha Afrika ya Maghribi zaidi kuliko hiki cha Nairobi. Watu wa Afrika ya Maghribi na watu wanoishii pwani katika Afrika ya Mashariki wanatumia masala mazuri sana.

Ninapenda kula chakula cha pwani. Napenda sana kombe ambazo zinaweza kupatwa hapa katika jimbo la California. California ina chakula na mboga nzuri sana. Napenda kwenda hotelini jijini San Francisco na kula pamoja na marafiki zangu.

Ninapenda pia kupika na kuandaa milo. Nikiweza kula mlo umoja kwa maisha yote ningekula chakula cha nchi ya Ethiopia. Napenda kula na mikono.

Kuna watu wengi wanaopenda kula vyakula vichache tu. Hawapendi kula vyakula vya ajabu na vigeni. Lakini ninapenda kula chochote. Ningejaribu hata kula dudu.

Kombe: oysters, shellfish

Unknown said...

Hilary, swali hilo ni nzuri zaidi. Pia, ni ajabu sana lakini hula chokoleti na nyama ya nguruwe wakati wengi! Ninakukubali kwamba chokoleti hii ni tamu zaidi kuliko aina nyingine ya chokoleti.

Ninavyopenda sana vyakula. Kuna vyakula fulani ambavyo ninahitaji kula mara mengi, kwa mfano maziwa lala. Kwa kawaida hula chakula hiki kila siku. Tokea hapo, nilikula maziwa lala kwa chakula cha jioni. Niliyaunga na aina ya nati inayoitwa “almond” na ya matunda zinazoitwa “blueberries”, “raisins” na “cherries”. Ninafikiri kwamba hakuna matunda haya pale Afrika ya Mashariki na ninapokuwa nipo pale ninayakumbuka matunda haya sana.

Kwa jumla, ninafurahia kujaribu vyakula mbalimbali. Kwa mfano, ijumaa, nilienda hotelini hapa San Francisco ambapo nilikula “bone marrow”. Bone marrow inaandalika na chumvi, dania na mkate. Pia unapata kijiko ili uweze kutoa nyama kutoka mfupa. Ilikuwa tamu sana. Chakula kinachopenda zaidi kinaitwa “brussels sprouts”. Hii ni mboga ninaochoma na mafuta, chumvi na pili pili. Hapa Marekani watu wengi wanazikula brussels sprouts wakati wa siku kuu ya asante na kabla ya Krismasi.

Ninapenda sana kupika hapa nyumbani, lakini ninapenda zaidi kula hotelini. Rafiki zangu nami tunakula katika hoteli mpya kila wiki mbili. Kila mara, mtu mmoja anachagua hoteli na hula pale pamoja. Kwa kawaida, tunaweza kujaribu vyakula vingi vipya kwa sababu tunapata vyakula mbalimbali ili tuweze kugawanya vyote.

Wiki ijayo nitatembelea jiji la New York, na hapo kuna vyakula vitamu zaidi. Nitakula “pork buns” (nyama ya tumbo ya nguruwe na mkate fulani), “biscuits” (mkate na unga fulani) na “bagels” (mkate tofauti unaochemsha na kuoka). Nitakuwa na furaha nitapokula vyakula hivi!

tokea hapo – actually
maziwa lala – yogurt
kuunga – to mix
nati – nut
kuandalika – to be served (stative)
mfupa – bone
kuoka – to bake

Rachel Quint said...

Asante sana kwa swali nzuri sana. Kama ninyi, ninapenda sana kula chakula, na ninapenda pia kupika chakula mpya.

Zamani, nilipokuwa kijana, nilikuwa nikikataa kula nyama kabisa. Nilikuwa "vegetarian" kwa miaka tano na nusu. Lakini, siku moja, baada ya miaka tano na nusu, nilitaka sana "hot dog" Sana. Halafu, nilikula "hot dog" mbili, na baadaye na sasa, ninakula nyama sana.

Ninapendelea kupika chakula cha sukari (nimekosa kutafuta neno nzuri kwa "dessert") kama keki, biskuti, nk. Mama yangu hapendi ninapopika kwa sababu ninapika chakula cha sukari, na halafu, ninaondoka, na mama yangua anakula chakula chote.

Baba yangu anapenda sana kula pia, na nimejaribu vitu kutoka sehemu za dunia ningi sana. Lakini, nikichagua chakula moja, nita chagua mkate na siagi kila siku, kwa chakula cha asabuhi, mchana, na jioni.

Ninazira chakula moja tu. Ninazira cilantro. Sana. Lakini, chakula chochote kingine ni sawa kwa mimi!