Friday, April 24, 2009

Unazitumiaje pesa zako?

Ninapopata pesa kidogo, kwa kawaida huzitumia kuwa na tajariba nzuri. Kwa mfano, hula pale hotelini tamu au husafiri katika nchi tofauti. Watu wananiambia kwamba nilinde pesa zangu kwa ajili ya wakati ujao ama ninunue nguo au vitu vingine. Je, unapopata pesa, huzilinda au huzitumia? Ukitumia pesa, unapendelea kununua vitu au kuzitumia kwa ajili ya tajariba maalum?

Na Lisa.

5 comments:

Rachel Quint said...

Maswali mazuri sana, Lisa!

Nilifanya kazi mbali mbali, lakini sijafanya kazi kwa muda ndefu. Halafu, sipati pesa kwa pepe (regularly?). Lakini, nikipata pesa, kwa kawaida, ninajaribu kulinda pesa yangu, lakini, kuishi ni ghali! Ninahitaji kununua chakula, nguo, na vitabu vya shule. Lakini, nikijua nina pesa ndogo, ninaweza kununua nguo ghali zaidi au kuenda hoteli.

Nina akounti ya ulinda, na nimeweza kulinda pesa ndogo. Halafu, nitahitaji kununua nyumba au gari, nitakuwa na ulinda wadogo.

Ningeipata pesa ningi sana, na ningeweza kutumia pesa kwa vitu vyote, ninafikiri ningetumia kurudi Tanzania. Au, ningetumia kwa safari y mimi na dada yangu. Ala! Bado sina pesa ningi!

Hilary said...

Maswali ya Lisa ni mazuri sana! Mara mengi, nimefikiri kuhusu masuala haya. Nina mawazo mawili. Kwanza, nafikiri bila shaka kwamba ni muhimu kulinda pesa kwa ajili ya kutumia ikiwa kuna dharurua au hali ya hatari, na kama una familia. Lakini, kwa mfano, Babu na Bibi yangu walilinda pesa zote zao bila kusafiri sana, na bila kununua vitu vizuri, na hata bila kuwapa watu wanaohitaji pesa. Sasa hivi, wao ni wazee na pesa haziwezi kufanya kitu chochote. Mwana na wajukuu wao hahitaji pesa hizi sana, kwa hivyo zinakaa benkini bila kutumika. Kwa sababu hii, nafikiri usilinde pesa zote. Sasa wazo wa pili: watu wengi husema tununue vitu ambavyo vinaweza kuishi daima kwani vitu hivi vina thamani nyingi. Lakini kitu ni kitu tu. Hakina maisha. Ni kitu ambacho tutumia au tuhakaza tu. Sijui nikiamini kwamba vitu vizure havina bei, au ni bure (kama penzi au ashiki), lakini nafikiri tajiriba na makumbuko ni kweli muhimu sana kuliko vitu tunavyoweza kugusa. Ikiwa “Scrooge” huunga pesa zake, mimi huunga makumbuko yangu. Pengine ninajisikia kama ninaweza kushuhudia makumbuko yangu tena na tena ninapofikiri kuhusu hayo. Kwa sababu hizi, mimi hupenda kulinda pesa chache na kutumia pesa zingine kufanya vitu sitawahivyosahau.

Michelle said...
This comment has been removed by the author.
Michelle said...
This comment has been removed by the author.
Michelle said...

Kwa kweli, nilipokuwa na pesa, hupenda kununua vitu vya sanaa, kama rangi, au kalamu nzuri, au karatasi ya rangi mbali mbali. Mwaka uliopita, nilifanya kazi kwa dada yangu, kuhifadhi mpwa wangu. Melissa alinilipa dolla saba kwa saa, halafu nilikuwa na pesa zaida kidogo. Niliporudi nyumbani, niliacha kwa soko la sanaa, kwa ajili ya kununua vitu vingi. Basi, nilienda kwa likizo fupi, kupaka rangi au kufanya vitu vizuri kutumia vitu vya sanaa vipya.

Nilipokaa Tananzania, ninapenda sana kutembelea soko la vitenge, kama barabara uhuru kando la Mnazi Mmoja. Pale, kuna vitenge vingi sana (na watu wengi sana pia!). Kweli, hapa vitenge ni ghali, kama angalau dolla tano kwa mita. Pale, nilinunua vitenge vingi, kwa sababu vitenge pale vilikuwa vizuri sana kuliko vitenge hapa, na rahisi sana pia kuliko vitenge hapa. Niliporudi nyumbani, niliipa familia yangu vitenge kama zawadi, na pia nilishona shiti mashiti kitanda changu pia. Hii ni picha!

pichakuhifidhi - to guard, protect, look after
zaida - extra, surplus, balance
shiti/mashiti - sheet(s)