Sunday, January 11, 2009
Tofauti kati ya biashara za zamani na za sasa baina ya Afrika ya Mashariki na sehemu za dunia nyingine
Kumekuwa na biashara kati ya watu wa Afrika ya Mashariki na sehemu za dunia nyingine (kama Arabian Peninsula au Southeast Asia) kwa miaka mingi. Je kuna tofauti gani kati ya ufanyaji wa biashara wa wakati huu na ule wa wakati uliopita (miaka mia moja iliyopita, kwa mfano).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Zamani wafanya biashara walikuwa wakisafiri kutoka nchi moja mpaka nchi nyingine. Kwa mfano, walifanya biashara viungo kwa sababu watu walioishi kando ya bahari walitaka viungo ili waweze kuviweka katika vyakula vyao. Pia, wakati mwingine, wafanya biashara walitafuta dhahabu, lakini hiyo ilikuwa ngumu zaidi kupata kuliko viungo.
Mwandishi wa vitabu vya anthropolojia - inaitwa Engseng Ho – anasimulia habari kuhusu jamii za wanazuoni wa dini waliokaa Hadramawt (katika nchi ya Yemen) na walisafiri katika bahari ya Bara Hindi ili wasome vitabu vya Uislamu katika mahali pengi na kufanya biashara na watu tofauti. Waliumba mitandao ya watu waliotoka Hadramawt na waliosoma Uislamu katika mahali kama vile Malaysia, Kenya, Tanzania, India, na kadhalika.
Kwa sababu hakukuwa na ndege watu hawa walisafiri kwa chombo. Walisafiri kwa siku nyingi kufika nchi nyingine. Sasa kwa sababu kuna ndege, watu wanaweze kusafiri kutoka nchi kama vile Kenya na kufika nchi nyingine kama India kwa muda mfupi kabisa. Kwa sababu ugunduzi wa mtandao, watu wengi wanaweza kuzungumza na watu wanaoishi katika sehemu nyingi za dunia. Hata wafanya biashara wanaweza kufanya biashara kutumia mtandao! Hawahitaji chombo kama watu waliosafiri miaka mingi iliyopita.
Msamiati mpya
chombo – sailing vessel, boat, dhow
kusimulia – to narrate, to recount, to tell
wanazuoni – scholars
kuumba – to make, to create, to form
ugunduzi – invention, discovery
Lisa ameankia vizuri kuhusi biashara za vitu zamani na biashara za sasa. Ninafikiri tofauti moja kubwa sasa ni biashara za utalii katika Africa Mashariki.
Zamani, biashara zilikuwa kati ya nchi ningine katika Africa sana. Lakini, sasa, kwa sababu utandawazi umeongeza, biasha ni kubwa zaidi -- kati ya Africa Mashariki na dunia nziba. Sehemu moja kubwa ni utalii, hasa waulaya na wamarekani.
(Ninajua sana kuhusu Tanzania kuliko Kenya, Uganda, nk, halafu nitaandika kuhusu Tanzania leo). Katika Tanzania, kuna mbuga za wanyama ningi na watu wengi wanapenda kufika Tanzania kuangalia wanyama wa porini. Pia, Zanzibar ni sehemu ya Zanzania ambayo watalii wanapenda sana kufika kupumzika porini. Sasa asimilia ishirina ya GDP ya Zanzibar ni fedha ya utalii.
Za mwisho, utalii itakuwa sehumu kubwa na kubwa zaidi ya Africa Mashariki. Halafu, biashara na uchumi utabadalika.
Msamiati mpya:
utalii -- tourism
utandawazi -- globalization
mbuga za wanyama -- animal parks/national parks
Sijui kuhusu biashara ya zamani, lakini nimeshangaa ilikuwa vitu vingi ambavyo vilifanya katika Tanzania. Haikuwa vitenge au kanga tu, vitu vingi hufanya katika Tanzania, kama mfuko, na chakula, na kadhalika. Labda ni tofauti kidogo kuliko Kenya, ninafikiri ni kwa ajili ya ujamaa.
Baada ya uhuru, Nyerere na TANU aliamua ilikuwa nzuri zaidi kwa Tanzania na kwa uchumi na mandeleo wa Tanzania kwamba vitu vingi vilifanya katika Tanzania. Kwa mfano, katika mwaka 1967, kiwanda cha vitenge “urafiki” kilifunga mjini. Walichagua jina la “urafiki” kwa sababu kiwanda kilijengwa na pesa za uchina. Viongozi vya uchina waliamua kwamba ni muhimu sana kusaidia nchi mpya kama Tanzania, hasa nchi ambayo ilichagua njia ujamaa, kama Tanzania.
Hata sasa, nilipofika Tanzania, niligundua kwamba historia hii ilikuwa dhahiri. Nilipoenda duka, kwa jumla chakula kilichouza kinatoka Tanzania. Pengine katika maduka kubwa (kama Shoprite) ninaweza kununua vitu vya Afrika Kusini au ulaya, lakini sikuweza kununua vitu kama hivi kila mahali.
dhahiri (adj) -- evident
Zamani watu wa Afrika ya Mashariki na Waarabu, Wachina, na watu wa Bara Hindi walikuwa wakifanya biashara. Miaka mengi iliyopita Waafrika ya Mashariki na Waarabu walikuwa na uhusiano. Lugha ya Kiswahili ina maneno mengi yanayotokea lugha ya Kiarabu. Kwa mfano Waswahili na watu wa ulfame wa Oman walikuwa wakiongoza misafara kwenda barani kuua tembo na kuokota pembe ya ndovu.
Baada ya uhuru nchi za Afrika za Mashariki zilikuwa zikifanya biashara na nchi za Marekani na Urusi kwa sababu nchi hizi zilikuwa zikipata nguvu. Wakati Vita Baridi kati ya Marekani ya Umoja wa Kisovyeti nchi ya Kenya iliyokuwa ikifuata ubepari ilikuwa ikifanya biashara na Marekani. Lakini nchi ya Tanzania iliyokuwa ikifuata ujamaa ilikuwa ikifanya biashara na Urusi na Uchina.
Sasa nchi za Afrika za Mashariki zinafanya biashara na nchi mbalibali sehemu za dunia nyingi. Kwa mfano serikali ya Kenya inafanya biashara na wanafanyabiashara ambao wanatoka nchi ya Libya, nchi ya Uyahudi, na jiji la Dubai. Vipande vya matatu (kwa mfano mota na magurudumu) vinatokea jiji la Dubai. Wakenya wachache hata wanasafiri jijini Dubai kuyanunua magari. Nguo za Kenya zinatokea Uchini na Marekani. Serikali ya Kenya inajaribu kuvuta uwekezajii wa kimataifa. Inashiriki na uchumi wa kimataifa.
Msamiati:
Kushiriki: to participate
Vipande: parts
Ubepari: capitalism
Pembe ya ndovu: ivory
Ulfame: kingdom
Kuongoza: to lead
Misafara: caravans, convoys
Magurudumu: wheels
Uwekezajii: investment
Nitalinganisha biashara kabla na baada ya ukoloni, ingawa si mwanahistoria. Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba usafirishaji ulikuwa tofauti na ugumu zaidi kuliko leo. Idadi kubwa sana hazikubebwa na wepesi. Bila shaka, kulikuwa na meli kubwa kusafiri baina ya Afrika na mahali zingine (hasa mashariki), lakini kwa bara, vitu vilisafiri taratibu.
Pia, Afrika hapakugawanyika na mataifa kama leo. Bila shaka, kulikuwa na viongozi na vyama vya watu, lakini badala ya mataifa, kulikuwa na makabila na ufalme, kwa mifano miwili. Kwa sababu hii, natumaini biashara baina watu yalitekelezwa na jinsi zingine kuliko sasa.
Tukumbuke kwamba bidhaa za kugusika hazikuwa pweke katika dunia ya biashara. Watu waliyabadilisha mawazo pia. Kwa mfano, dini inaweza kusafiri kwa meli au mikono na vitu vingine. Ndivyo, tunaweza kusema, zinaposafiri bidhaa, watu wanasafiri, na wanaposafiri watu, mawazo yanasafiri.
Ingawa biashara imebadili, Afrika hapajawahitengwa.
Msamiati:
ku*linganisha - to compare
usafirishaji - transportation
ku*gawanyika - to be divided
ku*tekelezwa - to be accomplished
bidhaa - merchandise/goods
-a kugusika - tangible
(ma)wazo - idea(s)
dini - religion
ku*tengwa - to be isolated
Post a Comment