Monday, May 25, 2009

Changamoto katika kujifunza Lugha.

Pengine, ni changamoto kuwasiliana katika lugha nyingine na watu wa utamaduni mwingine. Basi, utuambie kichekesho kuhusu kujifunza kufanya kitu au kusema kitu au kuelewa kitu katika Afrika Mashariki na katika Kiswahili. Chochote ni sawa, lakini ujaribu kutuchekesha! Kwa mfano, nafikiri niliwaambia watu wote kuhusu chakula cha asubuhi ambacho nilipika na sukari nyingi. Familia yangu ya Tanzania ilisema kilikuwa “kitamu sana!” lakini hawakukipenda na sikuelewa kwa sababu nilifikiri “tamu” ilifasiriwa “delicious” tu. Ninatumaini mimi si mtu pekee ambaye nimepata changamoto kama hii. Hebu tuelezee changamoto yako uliyokutana
nayo.

ku*wasiliana -to communicate

ku*fasiriwa -to be translated

3 comments:

Unknown said...

Nina kichekesho kizuri nituambie. Kabla ya kufahamu na kuongea Kiswahili vizuri, nilikaa pamoja na familia ya Afrika ya Mashariki. Wakati huo, sikuwahienda (unaweza kusema "sikuwahienda" ili kumaanisha "i had never"?) pale Afrika ya Mashariki. Sikufahamu vitu vingi kuhusu maisha na utamaduni pale hasa mashambani.

Basi, nilisoma pale na programu inayoitwa SIT (Chuo kwa ajili ya Mafunzo ya Kimataifa...School for International Training). Kwa wiki moja, wanafunzi wote ambao kusafiri pamoja na programu walihitaji kukaa na familia mashambani. Nyumbani kwa familia yangu kulikuwa mbali sana na mji ya Takaungu pale pwani ya Kenya. Kila siku, nilihitaji kutembea kwa miguu kwa saa moja ili kufika shule mjini. Nyumbani, hakukuwa na stima au maji safi. Hakukuwa na watu ambao waliongea kiingereza na sikuweza kuongea Kiswahili.

Siku moja, nilihitaji kujisaidia...nilijaribu kumuelezea "mama" yangu mambo haya, lakini nilifikiri kwamba yeye hakunifahamu. Yeye alinipa koleo na aliashiria mbali na nyumba. Nilichanganyikiwa kabisa kwa sababu sikutake kuwa mkulima, nilihitaji kujisaidia tu, lakini mara nyingi, mama alinipa koleo. Kwa sababu ya sikumfahamu, nilileta koleo mbali na nyumba na kusubiri kwa takriban dakika kumi. Nilihitaji kujisaidia bado, lakini mama yangu alikuwa na furaha niliporudisha koleo. Nilisubiri mpaka siku nyingine kujisaidia!

Baada ya tajariba hii, niligundua kwamba nilipaswa kujisaidia udongoni na kutumia koleo ili kuzika takataka yangu. Baada ya kujifunza hivyo, nilisikia aibu sana!


koleo - shovel
udongo - dirt, earth
kuzika - to bury
aibu - embarassment
kuashiria - to indicate, to signal to

Michelle said...

Tatizo langu mwaka uliopita ni saa. Mara moja, nilifika dukani karibu na Changanykeni. Ningelinunua bakuli kubwa kwa ajili ya kuchachaga nguo zangu. Nimeshanunua sabuni, lakini ninaweza kununua “bakuli kubwa” (sikujua neno la “ndoo” - tatizo la kwanza!). Basi niliuliza, lakini muzagi halikuwa na ndoo wakati hii. Saa alikuwa saa sita mchana. Lakini, ninasikia ni ngumu sana kufiriki “katika” masaa Kiswahili - halafu kwangu mimi ilikuwa “noon.”

Yeye aliniambia kurudi “saa tisa” kwa ajili ya kununua ndoo. Mimi, nilikuwa changanikiwa sana. Nilifikiri kwamba yeye aliniambia kusitasita masaa tisa, baada chakula cha jioni! Tulizumgumza sana, na hatimaye rafiki yangu, Lamis, alinisaidia. Yeyea alinieleza tofauti kati ya “masaa tisa” and “saa tisa.” Nilirudi dukani baaya ya masaa wawili, na nilinunua ndoo, na nikachachaga nguo zangu!

ndoo - bucket

Rachel Quint said...

Ninajua nina vichekesho vingi, lhalafu nitakuambia vichekesho vidogo vya tatu.

1. Kwanza, nilipofika Afrika Mashariki nilishangaa kabisa kwamba nilifikiri kuna baa ningi sana kwa sababu kuna "saloon" ningi. Lakini, nilijifunza kwamba "saloon" katika Afrika mashariki ni sawa sawa kama "salon" hapa Marekani. Halafu, nilijua kwamba kuna duka la nywele lingi, hakuna duka la pombe ningi!

2. Samahani kuhusu kichekesho hiki - lakini kwa kingereza kuna kitu kinaitwa "spork" ni uma na kijiko pammoja. halafu, tulijaribu kutanganeza neno la "spork" kwa kingereza, na tulisema "kijikuma"! Tuliona aibu kabisa.

3. Kwa kwisha, kabla ya nilijua kiswahili, sijajua neno "samahani" halafu, nilijaribu kusema "pole" lakini nilitaka kusema "samahani sana" na nilisema "pole pole" kila mara. Niliwachanganisha watu wengi.